Everton ndio ilikuwa timu ya kwanza kupata goli baada ya kiungo Ross Barkley kuifungia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 18 ya mchezo.
Kevin De Bruyne akaongeza bao la pili baada ya kuunganisha krosi ya kutoka upande wa kushoto iliyopigwa na Raheem Sterling, kisha Sergio Aguero kun, akahitimisha kazi kwa bao la tatu.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Goodson Park Everton walishindwa kwa ushindi wa mabao 2-1. Man City watachuana na Liverpool katika mchezo wa fainali utaofanyika Februari 28 katika dimba la Wembley.