Thursday, January 28, 2016

Aubameyang: Sikufurahia Kauli Ya Yaya Toure Kusema Sikustahili Kuwa Mchezaji Bora Afrika

Mchezaji bora barani Afrika’ Pierre Emerick Aubameyang kutoka nchini Gabon amesema hakufurahishwa na kauli ya Yaya Toure kusema kuwa hakustahili tuzo hiyo ya Glo-CAF.

Nilisikia uchungu sana na kile kilichosemwa,” alisema mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund. “Ni aibu.
Aubameyang alisema alisikitika zaidi baada ya Andrew Ayew pia kuhoji ushindi wake.
yaay
Tuzo hiyo ni ya mwaka mzima na sio kutokana michuano ya kombe la bara Afrika pekee,” aliongezea Aubameyang ambaye anaongoza kwa mabao katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani akiwa amefunga magoli 18.
Toure ambaye alitangazwa kuwa mchezaji bora wa 2015,alishinda tuzo hiyo kwa kipindi cha miaka minne iliyopita mfululizo.