Thursday, January 28, 2016

MAAJABU:Azikwa Na Kreti Za Bia Na Soda Kahama

Tukio hilo limetokea jana katika kijiji hicho baada ya mwanakijiji huyo, Mahushi Lutaja kufariki na baadaye familia yake kupitisha maadhimio ya kumzika na mali zake zote kwa imani ya kwamba kifo chake kimetokana na kurogwa na wao kuhofia kwamba wakibaki na mali zake nao watakumbwa na mauti.
Kwa mujibu wa diwani wa Kata ya Mwanase, Samson Masanja, Lutaja baada ya kifo chake alizikwa na baisikeli moja vitanda vinne na magodolo yake pamoja na masanduku ya nguo zake zote na vitu vingine vidogovidogo alivyokuwa akivitumia
Pia Masanja alisema, Lutaja alizikwa na makreti ya bia na soda ambayo kabla ya kifo chake alikuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya kuuza vinywaji kwenye kijiji hicho cha Mwamande ambapo tukio hilo limehusishwa na imani za kishirikina
Wakati akiugua ndugu zake waliamini kwamba ugonjwa huo uliopelekea kifo chake ulitokana na kurogwa hivyo familia yake iliingiwa na hofu hiyo hasa kutokana na kuwepo madai ya waganga wa jadi kuamini kwamba ndugu yao alirogwa