Wednesday, February 17, 2016

Huyu Ndiye Mfalme Mdogo Zaidi Duniani, Anatokea Uganda.

Leo Jumanne ya tarehe 16 Februari 2016 kwenye kipindi cha SUNRISE ya Times FM ilisikika stori juu ya Masuala ya Kifalme kama ilivyoelezwa na Stanslaus Lambat (mkutubi26) akiwa na Jeshi.
Alianza kwa kusema; Mnamo mwaka 1968 April 19 alizaliwa Prince Makhosetive Dlamini, ambaye wengi wanamfahamu zaidi kwa jina la “Mfalme Mswati III”… huyu alikabidhiwa Ufalme Mwaka 1986 akiwa na Miaka 18 tu na kwa Mwaka huo alivunja Rekodi ya kuwa Mfalme Mdogo zaidi Afrika, Mpaka sasa Mswati III ameshaoa rasmi wake 15 na ana Watoto takribani 30… Lakini nia yao haikuwa kumzungumzia sana huyo.
Nia yao ilikuwa kumzungumzia Mfalme wa Toro – Uganda anayeitwa “Rukirabasaija Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi IV” alizaliwa Mwaka 1992 na Aliupata Ufalme mnamo Mwaka 1995 (yaani akiwa na Umri wa Miaka Mitatu na Nusu tu), na aliupata Ufalme huo baada ya Baba yake Kufariki Dunia…
Ikumbukwe kuna wakati aliyekuwa Rais wa Uganda, Milton Obote alitupilia mbali maswala ya Kifalme lakini baada ya Yoweri Museveni kuingia Madarakani alirudisha Maswala ya Kifalme, Museveni inasemekana ni moja ya viongozi waliowahi kuonesha wazi kumpenda kijana huyu…
Lakini, Miaka kadhaa iliwahi kutokea wana ‘Toro’ ambapo anatokea Mfalme huyu walisema hawatampigia Kura Museveni kama hatowaomba msamaha baada ya Museveni kukaririwa akionesha kuchukizwa na Mfalme huyo jinsi anavyovaa na katika Maongezi yake alitamka Neno “This young Boy..” Neno hilo liliwakasirisha Wananchi wa Toro kwa kumuita Mfalme wao “Young Boy”, ingawa mambo hayo yaliihsa tayari.!
Mpaka sasa, Nyimba Kabamba Iguru Rukidi IV anashikilia Rekodi ya Kuwa Mfalme mdogo zaidi Duniani huku akiwa kwenye Kumbukumbu ya “Guinness Book of Records”.!
Nadhani unaelewa Mtu akisema Mtu fulani ni Mfalme, yaani kwa maana nyingine ni Kiongozi mwenye Mamlaka ya hadhi ya juu kwenye Jamii husika, ana Ulinzi wa kutosha ikiwemo Jeshi n.k, ana uwezo wa kutoa Amri, Maagizo Lakini pia ndiyeMtawala wa Ardhi husikana wengine humuita “LORD OF THE LAND”