Monday, February 8, 2016

Madaraja matano hatari zaidi duniani ya watembea kwa miguu, Afrika lipo hili pekee … (+Pichaz)

Mtu wangu wa nguvu bado millardayo.com inaendelea kukuletea kila linaloendelea duniani, iwe usiku au mchana, nimekutana na list nyingine ya TOP 5 ya madaraja hatari zaidi duniani ya watembea kwa miguu, hii ni list kutoka mtandao wa www.wonderslist.com.
5- Trift Bridge – Switzerland
Daraja hili lilijengwa mwaka 2004, na kukarabatia au kufanyiwa matengeneza kwa awamu ya pili mwaka 20o9, hili linatajwa kutokuwa daraja salama kwa binadamu kukatisha, kwani usalama wake mdogo sana, hata kamba zilizopo pembeni sio salama sana kuziamini kama zina msaada.
Neue TriftbrŸcke (Juni 2009), Trift, Kanton Bern, Schweiz
4- Musou Tsuribashi Bridge – Japan
Hili ni daraja ambalo lina miaka zaidi ya 50 toka litengenezwe mwaka 1950, limetengenezwa kwa bodi na kamba ambazo zinatajwa kuwa sio imara sana, hupitwa na watu mara kadhaa, ila unashauriwa kama unataka kufanya hivyo ni lazima ufikirie mara tatu kufikia maamuzi hayo.
Musou-Tsuribashi-bridge
3- Aiguille du Midi – Ufaransa
Daraja hili lipo Ufaransa na kama una matatizo ya moyo hushauriwi kuwa na mipango ya kupita daraja hilo, kwa sababu njia yake ni nyembamba na lina urefu wa futi 12600 kutoka usawa wa bahari, daraja hili ni tishio kwa kila mmoja kutokana na urefu wake.
Aiguille-du-Midi-France
2- Kakum National Park Canopy Walkway – Ghana
Daraja hili lipo katika hifadhi ya taifa nchini Ghana, lina urefu wa futi 76 kutoka chini na limetengenezwa kwa mbao na kamba, lakini daraja hili mara nyingi hupendwa kutumiwa na watalii. Hili ndio daraja hatari kwa watembea kwa miguu lilikuwepo Afrika.
Kakum-National-Park-Canopy-Walkway
1- Marienbruecke – Ujerumani
Licha ya kuwa kuna materio ya chuma baadhi yametumika kutengeneza daraja hilo ambalo lipo katika milima ya Bavarian na inaunganisha kati ya kilele cha mlima mmoja na mwingine, lakini sio salama. Kama utakatisha daraja hilo lazima mapigo ya moyo yaongezekea.
Marienbruecke-Germany