Wednesday, February 3, 2016

PICHA:HII NDO OFISI MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ NI SHIDAA

Katika maisha hakuna mtu anayejua baada ya uwepo wake duniani atakuja kuwa nani baada ya miaka kadhaa, na ndio maana kila mtu hujituma kutafuta ili kuwa na maisha mazuri baadaye.
Ndivyo ilivyo kwa mwanamuziki nyota nchini Diamond, ambaye amepitia katika magumu mengi katika kutafuta riziki lakini sasa anakula matunda yake kutokana na kile alichokiwekeza.
Katika hali ya kawaida ni vigumu kuona msanii akiwa na ofisi nzuri kama ya mwenyekiti mtendaji au mkurugenzi wa kampuni kubwa.
Kwa Diamond lakini, hamu yake ya kujibrand kuwa msanii mkubwa na wa kimataifa, imemfanya aamue kuwa na ofisi yenye hadhi yake

Kupitia mtandao wa kijamii nyota huyo anayetamba na ngoma ya ‘Utanipenda’ aeweka picha ya kwanza ya ofisi yake ya kuvutia baada ya mama yake kumtembelea.
Ameandika“Guess who Visited in my Office today!…. Mama Platnumz,” aliandika.
Hiyo ni ofisi ya kampuni yake ya WCB ambapo inadaiwa kujihusisha na masuala yote ya muziki wake lakini pia akiajiri vijana wapya kwaajili ya kuanza kushughulika na masuala ya upigaji picha za matukio mbalimbali, graphics na vingine.
Wakati huohuo staa huyo ameandika ujumbe wa kumpongeza Alicia Keys kwa kuzaliwa na kudai kuwa anampenda Keys, kutokana na jinsi anavyojitoa kwa ajili ya Afrika.
“The love and Support you give to Africa is what makes me be your Die hard fan of all time, apart from your Good Music…Happy Birthday Keys, May God bless you and your Family,” ameandika Diamond.