Wednesday, March 9, 2016

Ajali Mbaya Iliyohusisha Daladala na Malori Mawili Yaua Watu 4 na Kujeruhi 25 Jijini Dar es Salaam


Ajali Mbaya imetokea leo asubuhi eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam ikihusisha malori mawili  na daladala iliyo kuwa ikitokea Gongo la Mboto kuelekea Ubungo 

Kwa mujibu wa mganga mkuu Hospitali  ya  Amana, Dr Stanley Binagi, watu wanne wamefariki dunia huku 25  wakijeruhiwa.

Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugongana na Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.