Aajali ilivyotokea.Ng’ombe wakiwa wamkufa baada ya kugongwa na basi hilo.
Basi lapinduka na kujeruhi watu Igunga WATU kadhaa wajeruhiwa baada ya basi la Super Sami lenye namba za usajili T 819 DEN kutoka Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam kupinduka katika Kijiji cha Igogo, wilayani Igunga mkoani Tabora leo wakati likijaribu kukwepa ng’ombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa taarifa za awali zinaonyesha dereva wa basi alikuwa anaongea na simu.