Huenda ukitajiwa list ya majina ya baadhi ya wachezaji na mafanikio walioyapata katika vilabu vyao wanavyochezea, huwezi kuamini kusikia kuwa hajafanikiwa kushinda mataji makubwa na timu zao za taifa. Hii ndio list iliyotolewa na sokka.com
10- Luis Figo (Ureno 1991 – 2006)
Amefanikiwa kushinda mataji 23 kwa ngazi ya vilabu, akivichezea vilabu kama Sporting CP, Barcelona, Real Madrid na Inter Milan kabla ya kustaafu 2009. Amefanikiwa kufunga magoli 32 katika mechi 127 akiwa na kikosi cha wakubwa cha Ureno, licha ya kutajwa mchezaji bora wa FIFA 2001, hakuwahi kutwaa taji lolote na Ureno.
9- Dennis Bergkamp (Uholanzi 1990–2000)
Huyu ni nguli wa zamani wa Arsenal na Ajax, akiwa na Arsenal amefanikiwa kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu na mataji manne ya Kombe la FA, katika miaka yake 11 akiwa na klabu hiyo. Bergkamp hakufanikiwa kutwaa taji lolote akiwa na timu yake ya taifa yaUholanzi katika kipindi cha miaka 10.
8- Robert Baggio :(Italia 1988–2004)
Anatajwa kama mchezaji bora wa muda wote wa Italia, amecheza jumla ya mechi 489 na kufunga magoli 223 katika ngazi ya vilabu, lakini amefunga magoli 26 akiwa na Italia katika mechi 57, Baggio amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu, Copa Italia naUEFA akiwa na vilabu vya Juventus na AC Milan.
7- Michael Ballack : (Ujerumani 1999–2010)
Jina lake lipo katika list ya wafungaji bora wa muda wote wa Ujerumani, akiwa kaifungia jumla ya goli 42 katika mechi 98, jitihada zake hazikuwahi kusaidia kutwaa taji lolote akiwa na timu yake ya taifa ya Ujerumani, zaidi ya kufika fainali ya Kombe la dunia 2002 na kufungwa 2-0 na Brazil.
6- Cristiano Ronaldo (Ureno 2003 – )
Licha ya kutajwa kama moja kati ya wachezaji bora wa dunia kuwahi kutokea, Ronaldohajawahi kushinda taji lolote kubwa akiwa na timu yake ya taifa, Ronaldo ameishia kutwaa matahi yote makubwa ya ngazi ya vilabu akiwa na Man United na Real Madrid.
5- Lionel Messi (Argentina 2005 – )
Ndio mchezaji pekee aliyewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Ormara tano, amefanikiwa kushinda makombe 25 akiwa na FC Barcelona, yeye pia hajawahi kushinda Kombe la Dunia wala Kombe la Copa America.
4- Johan Cruyff: (Uholanzi 1966–1977)
Amefanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or mara tatu 1971, 1973 na 1974, ameshinda jumla ya mataji 23 akiwa na vilabu vya Ajax Amsterdam, Barcelona na Feyernoord, hadi anstaafu soka hakufanikiwa kutwaa taji lolote kubwa na timu yake ya taifa.
3- Paolo Mardini : (Italia 1988–2002)
Anatajwa kama moja wa mabeki bora kuwahi kutokea katika soka, amecheza katika klabu ya AC Milan na kustaafu soka 2009, Maldini ameshinda jumla ya mataji 26, yaani kashinda kila taji katika ngazi ya klabu, lakini timu ya taifa hana taji la kujivunia.
2- Ferenc Puskas : (Hungury 1945–1956)
Huyu anatajwa kama mfungaji bora wa muda wote kuwahi kutokea katika historia ya soka, amefunga jumla ya goli 84 katika mechi 85 akiwa na Hungary, lakini pia amefunga jumla ya magoli 514 katika michezo 529 akiwa na vilabu vya Budapest Honvéd na Real Madrid.
1- Eusébio: (Ureno 1961–1973)
Eusébio da Silva Ferreira anatajwa kama mchezaji bora wa muda wote wa Ureno zaidi ya Figo na Ronaldo, katika ngazi ya vilabu pekee amefunga jumla ya goli 749 katika mechi 745, lakini akiwa na Ureno amefunga jumla ya goli 41 katika mechi 64, Uzito wa jina lake ni ngumu kuamini kama hajatwaa taji lolote kubwa akiwa na Ureno.