Meja Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Benjamin Noah Msuya.
HAYA ni maajabu ya Mungu! Meja Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Benjamin Noah Msuya (74), amesimulia alivyougua jijini Dar, kwenda kutibiwa nchini Uingereza, alivyokufa, aliyokutana nayo ndani ya kifo na alivyofufuka.
Hayo aliyasema Machi 16, mwaka huu, nyumbani kwake, Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, alipoongea na gazeti hili.
Hayo aliyasema Machi 16, mwaka huu, nyumbani kwake, Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, alipoongea na gazeti hili.
Meja Jenerali, Benjamin Noah Msuya akiwa hoi kitandani.
MEJA JENERALI MSUYA NI NANI?
Mwaka 1979, Jenerali Msuya aliongoza majeshi ya Tanzania kuingia nchini Uganda wakati wa vita vya Kagera. Aliudhibiti mji wa Kampala na kumuondoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo, Idi Amini Dada.
Baada ya Idi Amini kukimbia, Meja Jenerali Msuya alitawala Uganda kwa siku tatu akisubiri kumwapisha Yusuf Lule kuwa rais mpya wa nchi hiyo.
Lule hakwenda sawa katika utawala, Msuya alitakiwa kumtoa na kumwapisha Godfrey Binaisa na baadaye Paulo Muwanga ndipo Msuya aliporejea nchini. Alistaafu jeshi kwa mujibu wa sheria mwaka 2001.

Familia yake.
Ana watoto watano, wa kike wawili. Sasa sikia simulizi yake nzito.
“ILIKUWA Desemba mwaka 2010, niligundua nina uvimbe mdogo upande wa kulia wa shingo yangu. Nilimwonesha mke wangu na binti yangu Eunice kitu hicho ambapo walinishauri nimuone daktari. Siku iliyofuata nilikwenda Hospitali Kuu ya Kijeshi (General Military Hospital) Lugalo, jijini Dar es Salaam, kumwona Kanali Dk. Mwanjela ambaye alikuwa akishu ghulikia faili langu la tiba.

Aliutazama uvimbe huo na kuniambia nisiwe na wasiwasi nao kwani ulikuwa ni uvimbe wa kawaida wa tezi. Nilikubaliana na ushauri wake kwani yeye ni daktari mwenye utaalam wa hali ya juu na wa muda mrefu. Hivyo, nilirejea nyumbani nikiwa sina wasiwasi kwamba nilikuwa ninaumwa.
Ilipofika Januari 2011, niligundua uvimbe mwingine mdogo chini ya sikio uliokuwa juu ya ule uvimbe wa mwanzo na nikagundua uvimbe mwingine tena juu ya upande wa kushoto wa shingo. Niliingiwa na wasiwasi na nikaondoka haraka kwenda kumwona Dk. Mwanjela ambaye alinitazama tena kwa makini na kunielekeza niende katika Idara ya Mionzi ambayo hushughulika na vipimo vya eksirei (X-ray) kwa ajili ya kufanya vipimo kwenye via vya uzazi.
Matokeo ya vipimo yalionesha hapakuwa na uvimbe mwingine ulioonekana zaidi ya ule uliokuwepo, yalithibitisha kwamba ule uliokuwepo ulikuwa ni uvimbe wa tezi tu ambao haukuwa na hatari yoyote. Kwa mara nyingine, niliondoka hospitalini hapo nikiwa na furaha.
Siku ya Machi 10, mwaka huohuo, nilisafiri kwenda Harare, Zimbabwe, na mke wangu Deborah, kwenda kumtembelea mkwe wetu wa kiume, Samuel Asamoah, ambaye ni mume wa binti yetu, Eunice, na ambaye ana watoto wawili wa kiume, Samuel Jr na Annabelle.
Huko tulipokewa vyema na kukarimiwa kwa kila kitu katika muda wote tuliokaa huko kwa mwezi mmoja. Tulifurahi sana kukutana na wajukuu zetu. Sam (Samwel) kila mara alirejea nyumbani kutoka ofisini akiwa na chupa ya pombe ya ‘whisky’, tena ile aina bora zaidi ya Johnny Walker. Ni aina ile ambayo ilikuwa katika chupa zenye kitambulisho cheusi, cha dhahabu na wakati mwingine cha bluu, ambayo ilikuwa ikiuzwa kwa Dola za Marekani 260 kwa chupa yenye ujazo wa lita moja.
Hapo nyuma, nilikuwa nimeamua kuacha kunywa pombe, si kwa ajili ya sababu za kiafya bali ni kwa vile niliishaingia katika umri mkubwa. Hata hivyo, niliupokea ukarimu huu kwa kufurahia kinywaji hicho na mjumuiko huo wa kifamilia.
Katikati ya Aprili mwaka huo, uvimbe uliokuwa kushoto mwa shingo yangu ulikuwa umeongezeka kwa idadi na ukubwa na pia ulianza kuuma. Usiku mmoja nilimwamsha mke wangu na kumwambia kuhusu maumivu niliyokuwa nayasikia na nikamwambia kwamba ikiwa nitakufa, basi itatokana na uvimbe huo.

Hivi sasa nafahamu ni kwa nini nilikisemea sana kitu hicho ambacho baadaye kilikuja kutokea. Baada ya wiki moja nilianza kuumwa kichwa, kusikia kizunguzungu na kichefuchefu kila mara. Niliacha kabisa kunywa pombe, nikawa nayadhibiti maumivu kwa kunywa vidonge vya ‘paracetamol’ na ‘aspirin’. Nilifanya hivi ili kabla ya kumaliza likizo yangu kabla ya kurejea tena kazini ili nimwone daktari wangu.
Siku ya Mei 10, tulirejea Tanzania na mara moja nikaenda kumwona daktari. Baada ya uchunguzi makini, daktari alipendekeza nikamwone mtaalam wa upasuaji ili aweze kuuondoa uvimbe mmoja kati ya ule niliokuwa nao aupeleke Hospitali ya Muhimbili ili kufanyiwa uchunguzi.
Nilipomwona Dk. Mlula, ambaye alikuwa ni mtaalam wa magonjwa hayo, alinikagua uvimbe huo na akashauriana kwa kirefu na wataalam wengine.
Nilipomwona Dk. Mlula, ambaye alikuwa ni mtaalam wa magonjwa hayo, alinikagua uvimbe huo na akashauriana kwa kirefu na wataalam wengine.
Je, kilifuatia nini? Usikose kusoma mkasa huu wa kweli katika Gazeti la Risasi Jumamosi siku ya Jumamosi.
Msikie akisimulia mwenyewe.