Wednesday, March 23, 2016

Ndugu 2 waliojilipua Brussels jana watambuliwa

1
Ndugu wawili waliojilipua katika milipuko ya kujitoa mhanga jana Ubelgiji Khalid na Brahim el-Bakraoui waliovaa nguo nyeusi. Mwingine kulia anadaiwa kuwa Najim Laachraoui aliyeshiriki pia kwenye shambulio la Paris, Ufaransa.
2
Najim Laachraoui mtuhumiwa wa ugaidi aliyehusika pia kwenye shambulio la Jijini Paris, Ufaransa.
3
Khalid El Bakraoui kabla ya kujitoa mhanga.
4
Ibrahim El Bakraoui akielekea kufanya shambulio uwanja wa ndege wa Brussels jana.
56
Taswira kutoka uwanja wa ndege baada ya milipuko miwili.
Malbeek train carriage.jpg
Kituo cha treni baada ya mlipuko.
8
Mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza kwenye kituo cha treni baada ya mlipuko.
WASHAMBULIAJI wawili wa kujitoa mhanga waliojilipua katika uwanja wa ndege wa Brussels jana (Jumanne)
wametambuliwa kuwa ndugu wawili, Khalid na Brahim el-Bakraoui.
Kituo cha runinga cha RTBF kimesema ndugu hao wawili walifahamika vyema na polisi.
Mwanamume wa tatu aliyeonekana kwenye video za kamera za siri zilizopo kwenye uwanja wa ndege akiwa pamoja na wawili hao bado anasakwa.
Milipuko miwili ilitokea katika uwanja wa ndege na mwingine mmoja katika kituo cha treni na kuua watu 34 na kujeruhi wengine 250.
Ubelgiji imeanza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
RTBF imesema ndugu hao wawili walifahamika na polisi na wana rekodi za uhalifu lakini hawakudhaniwa kuwa na uhusiano na ugaidi awali.
Kituo hicho cha runinga kimesema Khalid el-Bakraoui alitumia jina bandia kukodi nyumba katika eneo la Forest jijini Brussels ambapo polisi walimuua mtu mwenye silaha kwenye makabiliano wiki iliyopita.
Ilikuwa ni wakati wa msako huo ambapo polisi walipata alama za vidole za Salah Abdeslam, mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya 13 Novemba.
Abdesalam alikamatwa kwenye operesheni ya maafisa wa usalama Ijumaa.
Credit: BBC