Saturday, April 2, 2016

Angalia Hizi Picha Za Harusi Ya Dr Slaa, Sababu Za Kufanya Nje Ya Nchi,Na Alichosema Yeye Mwenyewe..


Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.
Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa moja, lakini habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani* akidai bado anamtambua Josephine* kuwa ni mke wake wake halali.
Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama impatie haki yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.

Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.
Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa kutokana na mapingamizi hayo.