Thursday, April 7, 2016

Mbunge Anunua Mabasi Kusafirisha Wanafunzi Bure...

Mbunge wa Mtwara Mjini Maftaha Nachuma (CUF) amenunua mabasi mawili kwa ajili ya usafiri wa walimu na wanafunzi katika jimbo kwake bure kwa lengo la kuwezesha kuinua kuwango cha elimu jimboni kwake.

achuma ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha HOTMIX kinahorushwa na EATV na kuelezea mikakati ambayo ameifanya kwa kipindi kifupi tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge.
''Nimenunua mabasi mawili kwa ajili ya jimbo langu na huu ni mshahara na marupurupu yangu lengo langu ninataka kwa kipindi nitakachokuwa Mbunge nihakikishe ninainua kiwango cha elimu katika jimbo langu na Mkoa wa Mtwara''-Amesema Nachuma.
Aidha Mbunge huyo amesema pia ameanzisha program inayoitwa ''Maftaha English Learning Program'' ili kuwezesha vijana ambao walifeli waweze kufundishwa na kujiunga na QT ili waweze kupata elimu na kwa sasa jimboni kwangu kumeanza kunukia kiingereza.
Pia Mbunge huyo amesema ameamua kujikita katika elimu zaidi kutokana na ukweli kwamba mikoa ya kusini watu wengi hawajanufaika na elimu kama ilivyo mikoa mingine nchini.
Kufuatia Mbunge huyo kufanya kazi hiyo atakuwa ameungana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwakusafirisha walimu bure katika jiji laDar es salaam, tofauti ni kwamba Nachuma yeye atasafirisha walimu na wanafunzi bure katika jimbo lake pekee.