Friday, April 1, 2016
Mshindi Wa Bss Kayumba Ataja Alipopeleka 50 Millioni Za BSS
Mmoja kati ya wasanii ambao kwenye Bongo Star Search 2015 alikuwa akipanda jukwaani kuanzia majaji mpaka washabiki waliopo ukumbini na hata waliopo majumbani walifurahi kila walipomuona alikuwa si mwingine ni kijana mdogo kuliko wote,kijana mfupi wa wastani ,mweupe kidogo huyu si mwingine ni Kayumba Juma "Katoto",ambaye kwa hivi sasa anatamba na nyimbo yake iitwayo katoto.
Jiji letu ikafunga safari mpaka Temeke Dar es salaam Tanzania ambapo kuna kituo cha mkubwa na wanawe ambapo hapo ndipo alipo kwa sasa .
Na haya ndio mahojiano:
Nasri:Mambo vipi Kayumba
Kayumba:Poa poa aje.
Nasri:Poa
Nasri:Kayumba ebu nambie historia ya maisha yako kiufupi
Kayumba:Anacheka kidogo,anhaa nina umri wa miaka 20 nimezaliwa 5/2/1996 anhaa kwa baba na kwa mama angu kote mimi ni mtoto wa kwanza ila kwa baba tumezaliwa saba na kwa mama watatu jumla tupo kumi
Nasri:Hebu nambie katoto ina maana gani
Kayumba:Anacheka kidogo,aah katoto ni jina langu la utani,kwenye instagram nilikuwa na hash tag katoto so kwa kuwa ilo jina katoto lilikuwa maarufu nikaona bora nyimbo yangu niite katoto.
Nasri:Kabla ya BSS ulikuwa wapi
Kayumba:Nilikuwa Manzese Mburahati nauza viatu na madela baada ya kuona kipaji changu kinapotea nikaamua kwenda mkubwa na wanawe
Nasri:Ulisoma mpaka kidato cha ngapi
Kayumba:Niliishia darasa la saba hapo nilifaulu kwenda form one bahati mbaya kutokana na hali duni ya maisha sikuendelea na shule.
Nasri:Baada ya kupata 50 millioni umezifanyia nini
Kayumba:Nashukuru m/mungu 50 millioni nimeitendea haki,nimemjengea mzazi wangu nyumba huko mbande na nimenunua gari si haba.
Nasri:Unapenda chakula gani
Kayumba:Wali nyama
Nasri:Diamond na Alli kiba unampenda nani
Kayumba:Enhee nawapenda wote
Nasri:Zari na Wema
Kayumba:Hilo sitaki kuliongelea kwa sababu hayanihusu
Nasri:Ahsante kwa ushirikino wako Kayumba karibu Dodoma
Kayumba:Anacheka kidogo....Ntakuja usijali
Na hayo ndio yalikuwa mahojiano mafupi kati ya Nasri na Kayumba Juma endelea kufatilia mahojiano ya wasanii wengine kutoka mkubwa na wanawe hapahapa Tchaoooooo