Wakati leo ndiyo siku ya harusi ya rapa Kanye West anayemuoa Kim Kardashian katika sherehe itakayofanyika Florence nchini Italia, msanii huyo wa kiume amesema mkewe mtarajiwa ni mzuri kuliko kipaji chake.
Jumla ya wageni 600 walikuwepo katika pati maalum iliyofanyika jana katika ukumbi wa Hall Of Mirrors ambako wawili hao walithibitisha kufanyika kwa ndoa yao leo.
Hata hivyo, katika sherehe hiyo, Best Man, Jay Z na mkewe Beyonce hawakuwepo, ingawa bvado kuna matumaini kuwa wapambe hao wa karibu wa wanandoa watarajiwa, watakuwepo harusini baadaye leo.