Monday, May 12, 2014

HII NDIO JEURI YA DIAMOND AKIWA KAZINI, JUA MTONYO ANAOBEBA NA SPEND YAKE AKIWA TOUR ZA NJE...SHUKA NAYO

Waandaaji wa show nyingi wametokea kumlinganisha sana umaarufu wa Diamond na Davido bila kupata jibu kamili, na kama unadhani ni wasanii wa nje tu ndio wenye mahitaji makubwa katika kufanya show zao, kama ulikuwa hujui basi hii, ukijua unaweza ukae chini na uanze kufikiria upya mtazamo wako, na hii ndio sababu Diamond Platnumz atazidi kuwa si msanii tu wa kawaida bali ni moja kati ya wasanii wengi wa kimataifa.
927682_738685642830175_1039120426_n
Mtonyo mpya anaochota Diamond katika show umetokea kuwapa shida waandaaji wa show,
Imeripotiwa wandaaji wengi wa nchi za nje wa matamasha, wadai kuwa, ingawa Davido ni msanii mkubwa sana kulingana na Diamond, ila mahitaji ya Diamond hadi kumpandisha kupiga show moja ni ya kutisha unaweza sema ni kama unamleta Jay-z.
12664_621974061157745_1042520019_n
Unaambiwa Davido yeye huwa unamwachia anachiw mtonyo wa shilingi 85 tu,ila kaa utulie usikilize mahitaji haya ya Diamond:
10326618_492301214231113_1344209867_nKwanza bila kumtonyesha kuanzia milioni 45 kwenda juu, utaishia kuongea naye kwenye simu tu, bila hata ya kuona sura yake, achana na hiyo basi kwanza kama umeshatenga hilo fungu na kufanikisha kumuita kupiga ku-sign contract yake, inabidi umsafirishe kwa private jet au first class plane, akishatua uwe umeshandaa presidential suit katika hoteli yeyote yenye hadhi ya nyota tano, kama ni Bongo ni Serena hotel pale kiroho safi, wakati huohuo uwe umashatenga vyumba maalumu vikubwa kwa ajili ya Dancers wake, vitu vingine ni watu kuwahudumia watu sita anaotembea naye, microphone ya pekee na vyakula atavyohitaji yeye, viwe teyari umeshaweka order vitengenezwe, kama anavyotaka yeye. Kama ulikuwa unamchukulia Dangote easy, jipange!.
1diamond