Tuesday, May 27, 2014

LUNGI WA BONGO MOVIE AACHIA MWILI WAKE WAZI KUONESHA TATUU..MTAZAME HAPA

MAKUBWA! Baada ya kujichora tatuu mbalimbali mwilini mwake, kuonesha amechizika kimalovee, mwigizaji Lungi Maulanga amechora moja yenye sura ya mpenzi wake ambaye hakutaka kumtaja.
Mwigizaji wa Bongo Muvi, Lungi Maulanga.
Akipiga stori na mwanahabari wetu, Lungi alisema kuwa ana tatuu 12 mwilini mwake ambazo alizichorea pande za Dubai alipokuwa ameenda kutembea lakini mahaba niue ndiyo yalimtuma achore hiyo yenye muonekano wa mchumba’ke.
“Tatuu zina maana lakini moja nimemchora mpenzi wangu na hata nikikutana na mwanaume yeyote anajifanya ananihitaji ajue kabisa ninaye nimpendae zaidi kwani tatuu hii siwezi kuifuta,” alisema Lungi ambaye amechafuka tatuu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye titi, paja na kiuno.