Monday, May 26, 2014

MAKAHABA WASTAAFU WAELEZEA JINSI BIASHARA HIYO INAVYOLIPA...SOMA ZIDI

WALIPOTIMIZA miaka 70, mapacha Louse na Matine Fokkens waliamua kustaafu kufanya biashara ya kujiuza mwili. 

Sasa hivi wana miaka 71 na wanaeleza siri ya kuwafanya wanaume wawe na furaha. "Nilichojifunza kuhusu wanaume ni kwamba wanakunywa pombe hawawi wazuri.

Nimejifunza pia wanaume wanawahitaji makahaba, ni kitu cha kawaida na lazima tuheshimu hilo,"anasema Louse mwenye watoto wanne.

Anaongeza "wanaume wamezaliwa hivyo kuhitaji kufanya ngono. Sioni tatizo kwa hilo na inanishangaza watu wanavyoshindwa kuheshimu kwa ukahaba tuliokuwa tukifanya".

Makahaba hao vikongwe wanasema katika kipindi cha biashara yao ya kujiuza mwili waliyoifanya kwa miaka 50, wameweza kulala na wanaume takribani 355,000.

Mapacha hao maarufu kwa kuvaa nguo nyekundu zinazofanana, walianza biashara ya `kujiuza’ wakiwa na miaka 20 baada ya kukimbia mahusiano ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia.
 
"Tulikuwa wadogo, tukipenda utani na tukiheshimu wanaume," anasema Louse. Madada hao waliofanya ukahaba jijini Amsterdam, Uholanzi wanasema siri ya kufanikiwa kwenye biashara hiyo ni kuwaridhisha wanaume kwa kila wanachotaka.

Wanaelezea zaidi siri ya mafanikio ya biashara yao kuwa wanaume wanapendelea vitu tofauti na kwa ubunifu hivyo wao wamekuwa wakijitahidi kuwatimizia hayo na kuwa wabunifu.

"Wanaume wengi wanaokwenda kwa makahaba wanafuata yale ambayo wake zao hawawezi kuwafanyia ingawa wanawapenda," anasema Martine na kuongeza:

"Siku zote unatakiwa uwe kama ulivyo. Hivyo ndivyo tulivyojifunza tangu tukiwa wadogo na hadi sasa na ni kweli imesaidia kwenye ukahaba".

"Tulikuwa tukikaa chumba kimoja na dada yangu na tukawa maarufu sana. Wakati huo hakukuwa na shoo za wazi, lakini sisi tulifanya kwa kucheza dansi," anasema Louse. Wanasema ingawa sasa wameacha biashara hiyo, bado wanavaa sana nguo nyekundu. Tangu wastaafu biashara ya ukahaba wamefungua duka la vitabu.

Wanasema karibuni wataonekana kwenye televisheni wakifanya biashara hiyo. Louse anasema kuwa haitamani tena kazi yake ya ukahaba na muda wake mwingi anautumia kwenye duka lake lililopo katikati ya mji wa Amsterdam wanapouza vitabu. Pia wamekuwa wakichora na kutokana na umaarufu wao wamekuwa na mawasiliano na watu wengi wanaokuja dukani kwao.

Louse anasema "Inabidi tufanye kazi sana kwa sababu hatuna pensheni kama ilivyo kwa wenzetu wenye umri kama wetu. Bado tunakutana na wateja wetu wa zamani, lakini si kwa biashara ya ukahaba ila tunakunywa wote chai au kahawa au tunakutana baa kupata pombe".

Louse anasema "Ukitaka kumpata mwanamume lazima uwe mwepesi kuzungumza naye na kumsikiliza anachotaka. Tulipoanza biashara hii kwenye miaka ya 1960 tulijifunza hili kutoka kwa wanawake wakubwa zetu tuliowakuta".


Mapacha hao wanasema wanaume wanaotoka nje ya ndoa zao wanataka kuwa huru na kufurahia tendo la ndoa. Hata hivyo wanashauri makahaba kuwakwepa wanaume wanaowafuata wakiwa wamekunywa pombe.