MWILI wa mwimbaji mahiri nchini aliyefariki dunia wiki iliyopita nchini Thailand, Amina Ngaluma ‘Japanese’ umewasili jijini Dar es Salaam jana usiku huu.
Nyota huyo wa zamani wa bendi mbalimbali nchini ikiwamo Double M Sound, African Revolution ‘Wana Tamtam’, mpaka mauti yanamfika alikuwa mwanamuziki wa bendi ya Jambo Survivors.
Kwa mujibu wa mume wa marehemu, Rashid Sumuni, msiba upo kwa wazazi wa marehemu Kitunda, Machimbo, Dar es Salaam ambako ndiko maziko yatafanyika hapo kesho mchana.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AMINA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!