STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amedaiwa kuukacha msiba wa aliyekuwa nguli wa filamu za Kibongo, Adam Philip Kuambiana na kujitetea kuwa alibanwa na majukumu.
Alipobanwa na mwanahabari wetu kuhusu kutohudhuria msiba huo uliodumu kwa takriban siku nne, Lulu alijitetea kuwa alikuwa Mwanza kikazi.
Alipobanwa na mwanahabari wetu kuhusu kutohudhuria msiba huo uliodumu kwa takriban siku nne, Lulu alijitetea kuwa alikuwa Mwanza kikazi.
“Nimebanwa na kazi, nipo Mwanza na kampuni yetu tunayofanya nayo kazi imetoa nafasi moja tu kurudi Dar kwenye msiba, nimeshindwa,” alisema Lulu.
Mastaa wengi walijitokeza kwenye msiba huo akiwemo Jacob Steven ‘JB’ ambaye alikuwa nchini Uturuki kikazi lakini akaziacha na kurejea Bongo kumpumzisha prodyuza wake.