Inspector Henry akiwasihi  mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti  wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya  taratibu za kesi.
********* 
Matukio ya ajabu yanayofanywa na mahabusu wanaoshinikiza kesi zao  kusikilizwa haraka ikiwa ni mbinu wanazoamini zitasaidia katika kile  wanachoeleza kuwa ni kudai haki zao yanaendelea kuonekana ambapo jana  mahabusu jijini Mwanza walifanya tukio la aina yake.Mahabusu wawili kati ya sita wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji jana  walijaribu kutoroka kutoka kwenye mstari wa utaratibu wa kuingia  mahakamani na kisha kung’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku  mmoja wao akivua nguo zote na kubaki mtupu.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa nne asubuhi katika Mahakama ya  Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza.
Thobias Warioba, mmoja kati ya mahabusu hao ndiye aliyevua nguo zote  na kubaki mtupu na kisha kupiga kelele akiwa ameshikilia mlingoti  akieleza kilio chake.
“Haiwezekani tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu  hazijasikilizwa. Wengine tumebambikiwa kesi. 
"Tunaomba haki zetu, polisi wanatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu mwaka 2011tulipokamatwa.
"Tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe.” Alisema Thobias Warioba.
"Tunaomba haki zetu, polisi wanatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu mwaka 2011tulipokamatwa.
"Tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe.” Alisema Thobias Warioba.
Inspector wa polisi alijitambulisha kwa jina la Henry aliwataka  watuhumiwa hao waondoke katika mlingoti na kuvaa nguo ili waingie  mahakamani kwani kitendo walichokuwa wakikkifanya ni kosa la jinai..
“Pamoja na maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili  ni kosa jingine la jinai, hivyo ni vyema mkaondoka kwenye mlingoti huu  na kuingia mahakamani. Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa.” Alisema Inspecta Henry.
 Askari polisi wakiwalinda mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji
 Inspector Henry (shati la  bahari) akiwa na Inspector Veda (mwenye koti) wakisikiliza hoja za  Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu akiwa  ameng’ang’ania mlingoti wa Bendera ya Taifa
 Ushawishi ukiendelea
 Mahabusu Thobiasi Warioba  (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu katu  waking’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza  kuzungumza na waandishi wa Habari.
 Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama.
 Mashuhuda






