
WAKATI msanii wa kizazi kipya anayefanya vizuri kwa sasa na kujizolea tuzo 7 alizokuwa anawania kupitia Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014, Naseeb Abdul 'Diamond akiibuka shujaa Mlimani City jijini Dar ambako hafla hiyo ya utoaji tuzo ilifanyika, usiku huo ulikuwa mbaya kwa mpenzi wake wa zamani,Jokate Mwegelo ambaye huenda alijuta kufika mahali hapo....
 Matukio   ambayo  yalimnyong'onyesha  Jokate  ni  namna  ambavyo  msanii  huyo   na  mpenzi  wake  Wema  Sepetu  walivyokuwa  wakionyesha  mahaba mazito   ukumbini  ilihali  yeye  akishuhudia....
Katika   hali  ya  kushangaza, Diamond  na Wema  kila  walipokuwa  wakichukua   tuzo  walikuwa  wakizunguka  nyuma  ya  jukwaa  ambako  alikuwepo   Jokate  na  kuzibwaga  tuzo  hizo  mezani  kisha  kukandamiza  'Denda  Live'  mbele  yake  kiasi  cha  kumfanya  mwanamitindo  huyo  ainame  kwa  Aibu....
Diamond   alionekana  kumpotezea  vibaya  mwandani  wake  huyo  wa  zamani  huku   Wema  akijikosha  kwa   kumpa  mkono  wa  kejeli  hali  iliyomfanya   Jokate  akose  raha  wakati  wote  alipokuwa  akiwaona  wapenzi  hao....
Matukio  ambayo  yalionekana  kumchoma  zaidi  moyoni  ni  jinsi Wema  alivyokuwa  akimvuta  Diamond  na  kubadilishana  mate  mbele  yake   jambo  ambalo  lilitafsriwa  kama  ni  kumfanyia  makusudi   mwanamitindo  huyo  ambaye  kipindi  cha  nyuma  alifanikiwa  kuleta   tafrani  kubwa  na  kuligawa  vipande vipande  penzi  la  wawili  hao   kiasi  cha  Wema  kulalamika  redioni....
Hali   ya  Jokate  kukumbwa  na   mfadhaiko  ilizua  minong'ono  kwa  baadhi   ya  mashuhuda  kwamba  Diamond  na  Wema  waliamua  kukata  kabisa   mzizi  wa  fitina  kwa  Jokate  na  kuudhihirishia  umma  kuwa  ya   kale  ni  dhahabu...
"Maskini   Jokate, ona  anavyofanyiwa  na  Wema,inauma  sana  moyoni.Unajua   mwanaume  kama  umewahi  kulala  naye  hata  mara  moja  ukiona   anafanya  mahaba  na  mwanamke  mwingine  inauma" Alisikika  staa  mmoja  akiteta  na  mwezake
Hadi   hafla  hiyo  inamalizika,Jokate  aliganda  kwenye  kiti  akiwa   amepooza  tofauti  na  ilivyo  kwa  staa  huyo  anapokuwa  katika   matukio  makubwa  kuwa  na  makeke