DIVA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameziomba mamlaka  zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii waigize nusu  uchi  ili kuendana na soko la kimataifa. 
Akitetea  hoja yake mbele ya mwandishi wetu, staa huyo aliyeitendea haki filamu ya  Foolish Age alitolea mfano Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa Lupita Nyong’o  ambayo alicheza akiwa nusu utupu.
“Wanasema hatufuati maadili wakati kuna muvi ambazo zipo theatre na  watu wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa  kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tuna takiwa tuweke vitu  wazi, wasibane sana,” alisema Lulu.