Mpaka sasa taratibu za mazishi ambazo zimetangazwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere kupitia exclusive interview na millardayo.com zinaonyesha Rachel atazikwa Alhamisi hii kwenye makaburi ya Kinondoni Dar es salaam.
Shughuli ya kuagwa kwa mwili itafanyika kwenye viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni na pia siku hiyo yatafanyika mazishi ya wote wawili yaani mama pamoja mtoto.
Shughuli ya kuagwa kwa mwili itafanyika kwenye viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni na pia siku hiyo yatafanyika mazishi ya wote wawili yaani mama pamoja mtoto.
Taarifa ya mwanzo ya familia ilikua marehemu akazikwe kwao Songea lakini kutokana na ushawishi wa waigizaji imebidi familia ya Rachel ikubaliane na ombi lao la maziko kufanyika Dar es salaam.
Hizi hapa chini ni baadhi ya picha kutoka nyumbani kwa marehemu maeneo Sinza Palestina.