Kama kawa wiki iliyopita tulimleta kwenu prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima ambapo mlimuuliza maswali anayoyajibu wiki hii. UNGANA NAYE… VIPI
KUHUSU BANGI?
Nasikia wakati unasoma ulikuwa unavuta bangi, je, ni kweli au? Andrew Kazala, Dar, 0717179570
SAUDA: Sijawahi kuvuta bangi na sijui inafanana vipi.
PONGEZI
Mara utasikia oooh, Maimartha Jesse anauza dawa za kuongeza makalio au Lulu Semagongo ana danguro la kuwauza mashoga lakini kwa Sauda Mwilima sijawahi kusikia skendo yoyote ile, hakika wewe ni kioo cha jamii hongera sana. Rocky Moshi, 0715289337
SAUDA: Nashukuru sana kwa hilo endelea kuniombea.
HUYU ANATAKA KUJUA
Sauda kwanza hongera kwa kuwa wewe siyo mtu wa matukio, nataka kujua eti ni kweli huwa unadaka mlungula kwenye kipindi chako cha Bongo Beat kwa wasanii? John Ipembe, Shinyanga, 0713554815
SAUDA: Hapana, kipindi changu ni kwa ajili ya kuwasaidia wasanii.
NINI AMBACHO HATAKISAHAU?
Jambo gani ambalo huwezi kulisahau katika maisha yako? Anijay Nswillah, Mbeya, 0768538920
SAUDA: Siwezi kusahau nilipompoteza mtoto wangu.
HUYU ANAMSHAURI
Nakushauri uache mkorogo utapendeza zaidi hukuwa hivyo zamani. Bland, Mwanza, 0782527646
SAUDA: Asante lakini situmii mkorogo.
ANA WATOTO WANGAPI?
Sauda nakukubali sana unavyotangaza naomba kujua umezaa na una watoto wangapi? Abuu Sungura, Dar, 0654799098
SAUDA: Sina mtoto.
ETI ALIWAHI KUWA RADIO FREE?
Dada Sauda mimi nakupenda sana kiukweli uko vizuri na unajitambua. Swali langu, je, uliwahi kuwa mtangazaji wa Radio Free? Raphael, Morogoro, 0713850820
SAUDA: Asante kwa kunipenda, ni kweli mpaka sasa ni mtangazaji wa Radio Free na Kiss FM.
JE, ANA NDOTO ZA KWENDA BBC?
Sauda ulishawahi kufikiria kufanya kazi BBC au ndoto yako imetimia kufanya kazi Star TV? Bforshizzle, 0713775834
SAUDA: Kila mtu ana ndoto za kuwa juu hivyo na mimi siku ikitokea hiyo nafasi nitamshukuru Mungu na nitaenda.
HUYU ANATAKA KUFAHAMU
Dada Sauda nakupongeza sana kwa kutokuwa na skendo, hongera, mimi ningependa kujua wewe ni mtu wa mkoa gani na je, umeolewa? Saidi, Dar, 0715155580
SAUDA: Nashukuru, mimi ni Mmanyema wa Kigoma, nimeolewa.
MALENGO YAKE
Hongera kwa kazi na changamoto zake, vipi matarajio yako ya baadaye? Frances Mwakibete, 0717274027
SAUDA: Malengo yangu ni kufanya kazi nzuri ili nifike mbali zaidi pamoja na kuelimisha jamii zaidi.
VIPI KUHUSU KANUMBA?
Eti inasemekana kuwa ulikuwa unatoka kimapenzi na mwigizaji nyota marehemu Steven Kanumba, je, kuna ukweli wowote na una umri gani mpaka leo kwenye fani ya utangazaji na unakumbana na vishawishi gani? Joel Kwanga, Dar, 0654066633
SAUDA: Sijawahi na Kanumba hakuwahi kunitamkia mambo ya mapenzi, nina miaka kumi kwenye utangazaji, vishawishi ni vya kawaida kwa kila mwanamke kikubwa ni kujitambua tu.
YEYE NA SAIDA VIPI?
Wewe na Saida Mwilima ni ndugu? Sasa hivi yupo wapi? Neema Wangwe, Dar.
SAUDA: Saida ni ndugu yangu tumezaliwa tumbo moja kwa sasa amehamia London (Uingereza).
CHANGAMOTO ANAZOKUMBANA NAZO
Naikubali sana kazi yako ila kuna changamoto gani unazipata katika kazi yako ya utangazaji? Baraka Suleiman, Dar, 0784613349
SAUDA: Changamoto ni za kawaida tu siyo nyingi.
ANA KAZI GANI NYINGINE?
Hongera kwa kazi, je, tofauti na kazi ya uandishi na utangazaji unajishughulisha na nini? Jose, 0757904855
SAUDA: Ninafanya biashara, pia ni mshehereshaji kwenye shughuli mbalimbali na mambo mengine mengi.
ANATAKA KUJUA
Tangu uanze mapenzi yenu na mume wako mlishawahi kugombana? Reshima, Dar, 0716258570
SAUDA: Hapana, hatujawahi kugombana, ikitokea ni vya kawaida tu vya kupishana kauli, tunaongea yanaisha, haijawahi kutokea ugomvi mkubwa.
HUYU ANAHOJI
Namjua dada Sauda alikuwa anaishi Morogoro maeneo ya Kigurunyembe karibu na Rombo Bar, baba yake alikuwa anafanya kazi kiwanda cha seramiki, ni mtu wa Mkoa wa Kigoma. Msomaji, 0712599020
SAUDA: Huyo ni dada yangu Saida, umetuchanganya.
ETI ALIWAHI KUSOMA DSJ AU TSJ?
Je, ni kweli Sauda uliwahi kusoma kati ya vyuo hivi DSJ au TSJ vilivyopo Ilala, Sharif Shamba, Dar? Muddy Madiley, 0652672805
SAUDA: Hapana sijawahi kusoma huko. NANI ALIMVUTIA KWENYE UTANGAZAJI?
Mimi nataka kujua ulianza lini utangazaji na nani alikuvutia kwenye fani hiyo? Rashidi Gombe, Dar, 0712231852
SAUDA: Nilivutiwa na dada yangu Saida, kipindi hicho nilikuwa shuleni yeye alikuwa Mtangazaji wa TBC kwa hiyo na mimi nilipomaliza shule nikafuata nyayo zake.