Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’
Matusi! Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutukanwa matusi ya nguoni na mwanadada anayejulikana kwa jina la Muna Alphonce kisa, kikidaiwa ni mwanaume.Habari ya mjini ilieleza kwamba Muna ambaye ni mke wa mtu aliporomosha matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini huku akimtoa kasoro mbalimbali Nisha na kumweleza kuwa hakuwahi kufikiria wala kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake wa sasa kwani ana mume na familia.
“Sina uhusiano na mwanaume wa Nisha ila kuna siku moja alinipigia simu na kujitambulisha kwangu kwamba anahitaji tufanye biashara kwani anafanya biashara ya magari lakini nikampotezea, akarudia tena mara ya pili pia nikampotezea lakini sasa nashangaa Nisha kudai ninamtaka mwanaume wake. Wewe nisha nikome kabisa,” alisema Muna.
Baada ya kuzinyaka habari hizo na matusi hayo ya nguoni, gazeti hili lilimtafuta Nisha na kumuuliza kulikoni ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi sigombei mwanaume na mtu. Mwanaume wangu ninampenda na yeye ananipenda japokuwa watu wanazungumza mengi,” alisema Nisha.