Monday, May 26, 2014

NJEMBA ‘AWAVUA’ NGUO WEMA NA AUNT EZEKIEL MCHANA KWEUPEE..BOFYA HAPA KUJIONEA

Mastaa wawili wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walikipata cha moto walipokuwa kwenye msiba wa Adam Kuambiana, Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar, baada ya kutukanwa na njemba mmoja aliyekuwa amelewa.

Mastaa wawili wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wakiwa katika Msiba wa Adam Kuambiana.
 Sakata hilo lilijiri usiku mwingi wakati  mastaa hao walipokuwa wameenda kulala kwenya matanga ambayo yalihudhuriwa na mastaa kibao, nyumbani kwa mke wa marehemu
Mwanaume mmoja (jina lake halikupatikana) alianza kumtukana Wema kuwa hana uzuri wowote kama walivyokuwa wakimuona kwenye runinga.

 Kitendo cha njemba huyo, kilimkera Wema na kuanza kujibishana naye, Aunt akaununua ugomvi na kujikuta naye akitemewa mbofumbofu.
Hata hivyo, mwisho wa sakata hilo Wema na Aunt waliamua kunyamaza kwani walibaini kuwa walikuwa wakijibishana na mtu ambaye ‘network’ yake ilikuwa bize kwa gambe