Sunday, June 29, 2014

BEYONCE AWASHANGAZA TENA MASHABIKI WAKE KWA KUFANYA HIKI KWA JUSTIN BIEBER

Beyonce-main
Tayari wamewashangaza mashabiki wao kwa kuonyesha video ya harusi yao iliyofungwa mwaka 2008 na kuzaliwa kwa mtoto wao Blue Ivy, sasa Beyonce na Jay Z wametoa mshtuko mwingine kwa mashabiki wao kwenye ziara yao ya muziki ya On The Run inayoendelea.
Bey na Jay Z waliwaonyesha mashabiki picha za mfululizo wa matukio yaliyomkumba mwanamuziki Justin Bieber hivi karibuni huku Beyonce akitoa kauli kwa mashabiki kuwa “Even the greatest can fall.”
Baadhi ya mashabiki walisema hiyo ni diss kubwa kwa Bieber ambaye amekumbwa na matukio ya kukamatwa mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni.
Mashabiki wengine walidai hiyo sio heshima kwa Justin Bieber huku wengine wakiandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa hilo ni funzo kwake sio tusi.