Baba wa mtoto Nasrah, Rashid Mvungi (47) akiingizwa mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada ya kupandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya kula njama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto Nasra.
Watuhumiwa wengine kwenye sakata hilo mama mlezi, Mariam Said (38) wa kwanza kushoto na mume wake Mtonga Omar (30) wa kwanza kulia wakisindikizwa mahabusu chini ya ulinzi wa polisi baada ya kusomewa mashitaka.
MTOTO Nasrah Rashid (4) aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kupata ulemavu kwa kufungiwa kwenye boksi miaka minne amefariki dunia. Nasrah alifichwa kwenye boksi na mama yake mkubwa aitwaye Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro tangu akiwa na miezi tisa baada ya mama yake mzazi kufariki. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!