Thursday, June 26, 2014

DIAMOND KUMRUSHA WEMA SEPETU KIMATAIFA..SOMA ZAIDI

Wema Sepetu anatarajia kufanya filamu mpya na wasanii kutoka Ghana ili kutanua wigo wake filamu pamoja na kwenda kimataifa zaidi.
Akizungumza na 225 ya XXL ndani Clouds FM, mpenzi wake na Wema, Diamond Platnumz amesema tayari ameshamfanyia mawasiliano na wasanii wa filamu wa Ghana ili kuhakikisha mwaka huu anafanya filamu ya kimataifa.
“Hapa juzi kati kulikuwa na mazungumzo, kuna mtu mmoja anaitwa Frank yupo huko Ghana, ni mtu mkubwa sana, na yeye ndio anaandaaga zile tuzo za Ghana, kwasababu kuna movie anataka kuifanya baby. Hiyo movie wajue kabisa eeh Sepetunga kaachia mashine mpya. So jamaa yule ana link na watu wengi nikajaribu kuzungumza kuwapata actors na actress ambao anaweza kushirikiana nao kwa sababu namna pekee ya kuweza kutanua market yako katika kazi yoyote ni kushirikiana na mtu ambae yupo katika nchi nyingine ili kuweza wewe kupenyeza bidhaa yako wewe na yeye apenyeze bidhaa yake kwako,” alisema Diamon.
wemadiamond
“Kama akina Van Vicker sijui akina nani, nimefanya mazungumzo nao kuangalia namna gani wanaweza kufanya movie na movie ifanyike Tanzania au ifanyike Nigeria au ifanyike Ghana. Ghana, Nigeria ni nchi ambazo zina nguvu kwenye soko la movie Afrika. Wakati nazungumza nao pia uzuri ilikuwa ni rahisi hivi baby kamlink sehemu yoyote ni rahisi sana kwa sababu kwanza ana content nyingi za movie zake. CV zake ni rahisi kumwambia mtu hiki na hiki, kwahiyo mtu akiona anashtuka, yaani mtu anakuwa excited kufanya naye kitu. So na wao pia kuna movie wanataka ashiriki uzuri pia wakasifika Kiingereza chake ni rahisi zaidi kufanya naye kazi. Kwahiyo mwenyezi Mungu akisaidia kuna mipango itakaa sawa basi mwaka huu utakuwa ni mwaka wake mzuri na zaidi nafikiri hata kabla hata mwaka haujaisha hii project itakuwa imekamilika labda inaweza kuwa out sijui yeye ndiyo anajua zaidi lakini. Wajibu wangu ni kutekeleza kuona kwamba baby amefanya movie na fulani na fulani kutoka nchi fulani na movie imekuwa fulani na kulingana alivyokuwa mwanzo na sasa hivi aonekane ame advance kutoka pale alipokuwa mwanzo.”