MNENGUAJI wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Maria Soloma amepigwa stop kuingia kwenye maonesho ya Bendi ya Mapacha Watatu kutokana na kitendo alichokifanya cha kumpiga chupa meneja wa Mapacha, Hamisi Dakota.
Chanzo kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, mwanadada huyo mara kadhaa amekuwa akitinga kwenye shoo za bendi hiyo akiwa amelewa na kumfanyia vurugu meneja huyo kiasi cha kuchafua hali ya hewa.
“Tukio la hivi karibuni la Maria kumvaa Dakota ndani ya Ukumbi wa Masai pale Kinondoni na kumrushia chupa iliyomjeruhi, Dakota aliona njia sahihi ni kwenda kumshitaki kwa bosi wake, Asha Baraka ambaye alimpiga marufuku demu huyo kwenda kwenye maonesho ya Mapacha,” alisema mtoa habari huyo.
Akizungu-mzia hilo, Asha Baraka alisema: “Ni kweli nimepata malalamiko ya Dakota akim- lalamikia Maria Soloma kwa tabia yake ya kwenda kwenye bendi yao na kuwafanyia fujo, hivyo kukomesha hilo tumeamua kumpiga marufuku kuhudhuria maonesho yote ya bendi hiyo,” alisema Asha Baraka.