Saturday, May 23, 2015

PICHA YA DIAMOND AKILA MISHIKAKI GUMZO

Stori: Musa Mateja
PICHA ya staa wa Nasema Nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayomuonesha akila mishikika uswahilini imezua gumzo la aina yake mitandaoni.
Staa wa Nasema Nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akila mishikika uswahilini.
Picha hiyo ambayo ilipigwa mwaka mmoja uliopita maeneo ya Tip Top, Manzese jijini Dar, imeibua mjadala mpya juzikati kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengine walimpongeza kwa kitendo hicho wengine wakisema si cha hadhi yake.
“Hii ni nzuri kwa mtu kama Diamond akila uswahilini. Anaonesha siyo mtu wa majivuno,” alichangia mdau mtandaoni huku wengine wakidai si sawa kwani anajiabisha.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Baada ya chanzo hicho kuipata picha hiyo na kumtumia mwandishi wetu, Mikito Nusunusu ilimtafuta Diamond ili aweze kuizingumzia lakini simu yake haikupatikana lakini Bab Tale alipatikana na kukiri maelezo ya chanzo chetu.
“Hakukuwa na ishu zaidi ya kuitamani mishikaki, tukaona tununue, mbona ni ya toka mwaka jana?,” alisema Bab Tale