Saturday, May 23, 2015

ZARI ATESWA NA PICHA YA KATUNZI

Mchumba wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’,  Zarina Hassan ‘Zari’.
MUSA MATEJA
MCHUMBA wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’,  Zarina Hassan ‘Zari’ amedaiwa kuangua kilio baada ya kuvuja kwa picha yake na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Mzamili Katunzi ambayo ilidaiwa kuwa ni mtu wake na kusababisha gumzo mjini.
Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa na pedeshee maarufu Bongo, Muzamili Issa Katunzi.
Mtu wa karibu na Zari amefunguka kuwa Zari alijisikia vibaya sana baada ya kuona picha hiyo na kukasirika hivyo kuanza kuwasaka watu walioivujisha kwani walikuwa na nia mbaya ya kumgombanisha lakini wamechemka.
“Zari kamaindi kweli, anajiuliza huyo aliyeivujisha alikuwa na lengo gani?” alisema mtu huyo.
Supastaa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’.
Jitihada za kuzungumza na Zari hazikuzaa matunda lakini bahati nzuri Diamond alipatikana na kufafanua:
 “Ni kweli zimemsumbua baby lakini nimemuweka sawa kwa kuwa najua ni mambo ya mitandao, hakuna ukweli wowote.”