Tuesday, June 24, 2014

HATIMAE YULE MWANAMKE WA KISUDANI ALIYEHUKUMIWA KIFO KWA KUIKANA DINI YAKE BAADA YA KUOLEWA NA MKRISTO AACHIWA HURU

mwanamke
Kwa mujibu wa BBC, Mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kosa la kuikana imani ya dini yake na kuolewa na mwanaume anayempenda wa kikristu amechiwa kutoka gerezani.
Shirika la habari la Suna limeripoti kuwa, hukumu ya kifo iliyotolewa kwa mwanamke huyo Meriam Ibrahim ilibadilishwa na mahakama ya rufaa
Mwanamke huyo aliolewa na mwanaume wa kikristu na alihukumiwa kifo kwa kutumia sheria za kiislamu Sharia baada ya kukataa kurejea kwenye dini yake.
Mume wake amesema kuwa anatarajia kumuona mke wake akirejea nyumbani.
Aliwekwa gerezani tangu February mwaka huu akiwa na mtoto wake mdogo wa kiume aliyejifungua akiwa ndani.