Hii ni moja kati ya zile kesi za kanisa katoliki zilizodumu kwa muda mrefu sana manake hii ilianza toka mwaka 2007 pale ambapo serikali ya nchi hii ilitishia kulifungia gazeti la kanisa hili kama lingeendelea kumuita Mungu Allah.
Taarifa mpya ya sasa inasema Mahakama kuu nchini Malaysia imetupilia mbali ombi la kanisa katoliki nchini humo kumuita Mungu ‘Allah’ kwenye gazeti hili linaloandika habari zake kwa lugha ya Ki malay.
Walidai kuwa Wakristo wanawakanganya Waislamu walio wengi na hilo laweza kuhatarisha usalama wa taifa ambapo uamuzi wa Mahakama ni mojawapo ya mikondo ya mwisho ya kesi za kisheria za kanisa katoliki zilizochukua muda wa miaka saba na kusababisha mashambulizi katika makanisa, majumba ya maombi ya waislamu na pia hekalu la wasikh mwaka 2010.
BBC wanaripoti zaidi kwamba Wakristo na wasikh wanadai kuwa wamekuwa wakimwita Mungu ‘Allah’ katika lugha za kiMalay na Sansrit kwa muda mrefu sana.
Mahakama nayo imeshikilia uamuzi wao wa awali kuwa jina hilo halifai kuingizwa katika ukristo ambapo mgongano huu kuhusu neno hilo moja umedhihirisha jinsi nchi hiyo yenye dini na kabila tofautitofauti lilivyogawanyika.
Wanaharakati wa kiislamu wamekua wakishabikia uamuzi huo nje ya Mahakama huku wengi wao wakiwa wanaamini kuwa wakristo wanamwita Mungu ‘Allah’ kama njia ya kuwavuta waislamu wajiunge na ukristo, shutma ambazo wakristo wamekana.