Tuesday, June 24, 2014

UKATILI, KICHANGA CHATUPWA KWENYE DAMPO LA TAKA..SOMA ZAIDI


Kichanga kinachokadilwa kuwa na umri wa miezi kati ya 6-7 kimekutwa kimetupwa kwenye dambo karibu na mahakama ya mwanzo mkabala na ofisi za manispaa ya Iringa, mkoani Iringa na mwanamke mmoja ambaye hakufahamika mara moja leo.

Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema wanamtafuta mwanamke aliyefanya kitendo hicho ili sheria iweze kuchukua mkondo wake pamoja na kukomesha vitendo hivyo mara moja .