Friday, June 6, 2014

Huyu ndiye Chatu aliyeuwawa Arusha Mchana wa June 05,kuna picha zake 5 hapa.

CHA1

Wiki chache zilizopita wakazi wa Kinondoni walimuua Mamba ambaye alikua akiishi karibu na bwawa maeneo ya Kinondoni block 41 na ni baada ya kuchoshwa nae wakaamua kumuua,sasa baada ya mamba hapa kuna stori ya Chatu aliyeuwawa Arusha.
Kwa mujibu wa Arusha yetu Blog wanasema kuwa Chatu huyo aliuwawa na wananchi mchana wa June 05 na ni baada ya kuonekana  maeneo ya Sakina Arusha akiwa amefungwa kitambaa chenye maaandishi mekundu.
Wakazi wa eneo la Sakina wamepatwa na mshtuko mkubwa,kikubwa zaidi kwa Chatu huyo ni kuwa inasemekana alionekana akiingia ndani.
Mara baada ya kuonekana kwa Chatu huyo wananchi walijipanga kisha wakafanikiwa kumuua ingawa kulitokea utata baada ya Mama mwenye nyumba aliyetokea Chatu huyo kupinga kuuliwa kwa Chatu huyo,Chatu huyo aliuwawa kisha akakatwa vipande vipande.

CHA4
CHA3
CHA2