Tuesday, June 24, 2014

KUMBE HIKI NDICHO KILICHOMFANYA WEMA KUNYOA UPARA....BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

Kumbe hiki ndicho kilichomfanya Wema kunyoa upara.


Wengi walikuwa wanajiuliza kunani, haswa siku Wema Sepetu alipoamua kunyoa Dongo, huku kila mtu akitoka na story yake mwenyewe kwa mtazamo tofauti bila hata kujua sababu halisi ya uamuzi wake huo, ila ukweli ni kwamba, 

Diva huyu ni moja kati ya wasanii wanaochukua kazi yake very serious, na hii ndio siku alipoamua kupotezea urembo wake na kuvaa uhusika wake uliomlazimisha kuchukua hatua hiyo ya kunyoa Upara, 

Akiwa anaongea katika nyakati tofauti alisikika akifunguka kuwa, Movie mpya yake anayoifanya iitwayo Family ndio iliyomfanya anyoe upara, huku akielezea kuwa ilimbidi kufanya hivyo kutokana na uhusika aliotakiwa kuvaa, uliokuwa unaelezea mtu mwenye Saratani.
 Wema ni moja kati ya wasanii wachache ambao hadi hii leo wana uwezo wa kufanya hivi ili tu kufikisha maudhui ya story iliyokusudiwa kwa jamii