Sunday, July 6, 2014

DUDU BAYA AKANUSHA KUTISHIA KUMKATA MASIKIO MPENZI WAKE


Rapper Godfrey Tumaini aka Dudu Baya amekanusha taarifa zinazosambazwa na mpenzi wake kuwa anamtishia kumkata masikio pamoja na kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kijana anayetambulika kwa jina la Aunt Bilal.

Akizungumza na Bongo5 leo, Dudu Baya, amesema kuwa mpenzi wake huyo ambaYe pia ni mganga wa kienyeji anatapatapa kutokana na maumivu ya kuachwa.

“Huyu demu ameachwa mara tano, ana matatizo ya wivu, pia huwa anatishia ukimwacha atakuroga, alishawai kuwa na mzungu na wakazaa huyo mzungu alimkimbia bila hata kuaga akaenda Marekani,”
amesema Dudu. “Mimi hajanifukuza kwake nimeondoka mwenyewe na nilimuaga nikamdanganya naenda Morogoro, hata mimi nashangaa nimkate masikio kwa sababu gani? Siwezi kufanya hivyo, eti nina mahusiano na Aunt Bilal, haiwezekani! Polisi wamemuambia asikimbilie kwenye vyombo vya habari haya ni mapenzi, achana na hasira tuwasuluhishe, mimi nikasema haiwezekani niambie mimi nawachukua mademu nafanya nao mapenzi chooni? Haya ni mambo ya kuchaufana tu, hakuna ukweli wowote, nimezunguka kwenye tour nyingi nimewahi kuandikwa kuhusu tuhuma kama hizi, mimi nawaomba watu waangalie ukweli uko wapi, mimi siwezi fanya vitu kama hivyo,” aliongeza