Friday, July 4, 2014

FACEBOOK KUCHUNGUZWA...NI BAADA YA KUWAFANYIA WATU UTAFITI WA KISAIKOLOJIA BILA YA WAO KUJUA


Facebook imekana kuwa ilikusanya taarifa za watu kisiri
Tume inayodhibiti taarifa za umma nchini Uingereza inafanya uchunguzi iwapo mtandao wa Facebook ulivunja kanuni zinazolinda data ya watu binafsi.
Hii ni baada ya taarifa kuibuka kuwa Facebook iliwafanyia watu utafiti wa kisaikolojia bila idhini yao.

Afisi ya mkuu wa habari wa tume hiyo alisema kuwa kuwa shirika hilo lilikuwa limepanga kuihoji Facebook kuhusu utafiti huo.Katika utafiti huo, Facebook ilichunguza taarifa za watu wapatao 700,000 ili kudhibiti hisia ilizotaka kutoka kwao.

"Tunafurahia kujibu swali lolote walilo nalo wadhibiti," Richard Allen wa Facebook alisema katika ripoti moja.
Majarida ya 'The Financial Times' pamoja na 'The Register' yalinakili kuwa afisi hiyo ilisema kuwa ingewasiliana na shirika la kudhibiti data la Irelend kuhusiana na swala hilo.
Facebook ina moja ya makao yake jijini Dublin.
'Utafiti wa Hisia'
Utafiti huo uliendeshwa pamoja na chuo kikuu cha Cornell na vile vile chuo kikuu cha Carlifornia jijini Sao Paulo kwa watumizi 689,000 wa Facebook kwa muda wa juma moja mwaka wa 2012.
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo: "uchunguzi huo uliendeshwa kwa kiwango ambacho taarifa za faragha za watu zilifichuliwa.''
Utafiti huo ulionyesha kuwa watumizi waliokuwa na taarifa chache hasi katika mtandao wao hawakuandika kwa urahisi taarifa mbaya, na kinyume chake.
Kadhalika utafiti huo ulifanywa ili kupima iwapo "tabia ya mtu kuandika katika ukurasa wake wa facebook unaathiriwa na hisia zake."
Hata hivyo, utafiti huo umekosolewa kwa sababu watumizi wa Facebook hawakujuzwa kuwa walikuwa wakihusishwa.
Mbunge wa chama cha Labour Jim Sheridan, mwanachama wa kamati ya uanahabari ya Commons media select, ametoa wito kwa uchunguzi kufanywa kuhusu swala hilo.
'Kuboresha taratibu zetu'
Kwa upande wake, Facebook imejitetea kwa kusema kuwa utafiti huo haukuhusisha ukusanyaji data wa watu usiohitajika."
"Hakuna data iliyotumiwa iliyohusiana na akaunti ya mtu yeyote maalum," ilisema Facebook
Siku ya Jumanne, bwana Allen alisema: "Sasa ni wazi kuwa watu walikasirishwa na utafiti huu na tumewajibika."
"Tunataka kufanya bora zaidi siku zijazo na kuboresha taratibu zetu kutokana na maoni haya."
Wakati huo huo, Adam Kramer wa Facebook, ambaye pia alihusika katika kutoa taarifa kuhusu uchunguzi huo , amekiri kuwa kampuni hiyo haikueleza "vizuri nia yao katika ripoti yake."

"ninaelewa ni kwa nini watu kadhaa wameonyesha hofu yao kuihusu, na waandishi wenzangu pamoja nami tunaomba radhi kwa jinsi ambavyo ripoti ilieleza utafiti huo pamoja na wasiwasi iliyosababishwa," alisema mapema wiki hii