Thursday, July 3, 2014

MAJAMBAZI YAVAMIA KWA KULISHAMBILIA KWA RISASI BASI LA MAGEREZA WAKITAKA KUWAOKOA WENZAO

WATU wanaosaidikiwa kuwa majambazi wameshambulia kwa risasi basi la Jeshi la Magereza likiwa na watuhumiwa mbalimbali wakiwamo majambazi sugu na kujeruhi askari wawili.
Habari za uhakika zimeifikia FikraPevu kuwa tukio hilo limetokea muda mchache Jumatano Julai 2, 2014 eneo la Mikocheni karibu kabisa na hoteli ya Regency, wakati basi hilo likiwa njiani kutokea mahakama ya Kawe kurudisha watuhumiwa gerezani.
magereza

Askari magereza walifanikiwa kuondoka na watuhumiwa hao na haijafahamika mara moja hatima ya majambazi hao.
 
Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea.
CHANZO: Fikra Pevu