Tuesday, August 19, 2014

JE WAJUA??HIVI NDIVYO VIWANJA VYA NDEGE VITANO BORA ZAIDI AFRIKA.

1. OR TAMBO INTERNATIONAL AIRPORT  (ORTIA), JOHANNESBURG - AFRIKA KUSINI.

Kiwanja hiki ndicho kiwanja bora zaidi Afrika na kina uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu Milioni 17 kwa mwaka na kwa sasa kiwanja hiko kimefanyiwa marekebisho na kuongezwa miundo mbinu na kukifanya kiweze kuhudumia zaidiya abiria Milioni 28 kwa mwaka.
Hata hivyo, ORTIA ndicho kiwana kikubwa zaidi cha ndege na pia kilicho na pilikapilika nyingi kabisa Afrika na pia kiwanja hiko kina wafanyakazi zaidi ya 18,000 walioajiriwa kiwanjani hapo na makampunim tofauti tofauti. Jina la kiwana hiko limetoka na aliyekuwa akipinga masuala ya ubaguzi wa rangi Afrika ya kusini kipindi cha makaburu aliyejulikana kama Oliver Reginald Tambo kama kumuenzi.
2. CAPE TOWN INTERNATIONAL AIRPORT, CAPETOWN - AFRIKA KUSINI.


Kiwanja hiki kipo Capetown Africa ya kusini na ifikapo mwaka 2015 kitakuwa kina hudumia zaidi ya Abiria Milioni 14 na pia kiwanja hiki hutumika sana kwa ajili ya shughuli za kitalii kwasababu mji wa Capetown una vivutio vingi vuya utalii nchini humo.
3. KING SHAKA INTERNATIONAL AIRPORT, DURBAN - AFRIKA KUSINI

Kiwanja hiki kilifunguliwa mnamo mwezi Mei 2010 na pia kina julikana kwa jina la LA MERCY AIRPORT kipo kilometa takriban 35 kaskazini kutoka katika mji wa Durban. Pia inasemekana kiwanja hiki ni kikubwa mara tatu zaidi ya Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Durban (Durban International Airport).
4. CAIRO INTERNATIONAL AIRPORT, CAIRO - MISRI


Hiki ni kiwanja cha ndege kikubwa zaidi Misri na ni cha pili kwa kuwa na pilika pilika nyingi za watu na pia zaidi ya ndege 65 hutumia kiwanja hiko kwa mwaka.
5. HURGHADA INTERNATIONAL AIRPORT, HURGHADA - MISRI


Kiwanja hiki kinajengo la abiria moja tu ambayo inafanya kazi kwa sasa na pia kinaongezwa kinaongezwa jengo lingine la abiria ambalo litakifanya kiwanja hiki kiweze kuhudumia zaidi ya abiria milioni 7.5 kwa mwaka.
Hata hivyo ni zaidi ya ndege 40 hutumia kiwanja hiki kwa mwaka.deee