WAKATI mastaa hupendelea kufanya shopping katika maduka makubwa, msanii wa filamu Miriam Jolwa maarufu kama Jini Kabula, mwishoni mwa wiki iliyopita alinaswa akichagua gauni alilodai ni la harusi katika duka la mitumba lililopo Makumbusho jijini Dar.
Msanii wa filamu, Miriam Jolwa maarufu kama Jini Kabula akiwa na rafiki yake Isabela wakifanya shopping katika duka la mitumba.
Msanii huyo akiwa na rafiki yake, Isabela walikutwa wakiwa bize katika duka hilo linalofahamika kama kwa Mzee wa Pamba.
“Kwani kuna ajabu gani mimi kuja kununua gauni la harusi yangu mtumbani? Watu wanashidwa kuelewa kuwa magauni ya mitumba ni mazuri sana” alisema baada ya kuulizwa kulikoni asiende kwenye maduka makubwa ya nguo.