Jux amekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake Vanessa Mdee na kudai kuwa Vanessa ni mshikaji wake tu lakini amekiri kuwa muimbaji huyo wa ‘Come Over’ ana kila sifa ya kuwa mke.
Jux ambaye hivi karibuni alionekana kuwa karibu na Vanessa amesema Vanessa ni mtu wake wa karibu anayefanya kazi naye. “No ni mshikhaji wangu tu, tunafanya naye kazi, kuna tabia zinaendana, kama ninavyokuwa na rafiki na Stamina, Mo Music ni kawaida, sema unajua ni mwanamke na ni njia toafuti ndio maana imekuwa hivyo,” alisema Jux.
Alipoulizwa kama Vanessa anafaa kuwa wife material Jux alijibu Vanessa ana kila sifa ya kuwa mke.
“Ni msichana mzuri, mwonekano wake mzuri, she is smart, yeah she is a wife material, yuko vizuri, lakini na mimi tumeendana sana tabia zetu kama washikaji. Sema nipo naye karibu na kwa sababu mimi sionekanagi na wasichana wengi ndio maana imekuwa hivyo. Lakini sijui labda baadaye kwa sasa hivi ni mapema, vyote anapanga Mungu,” alisisitiza Jux.