Monday, August 18, 2014

MSANII WA BONGO MOVIE MAYA ATAMBA KUWA HAJAPOTEZA BADO KWENYE GAME

mwigizaji wa sinema za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa watu wanaomsema kuwa amepotezwa kisanaa wanamkosea kwani anafanya sanaa kwa malengo.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’.
Maya alitoa kauli hiyo wikiendi iliyopita baada ya kusambaa kwa taarifa mitandaoni kuwa amepotezwa kisanaa na wasanii chipukizi kiasi cha kumfanya asisikike kama zamani.
“Sijapotezwa, kwenye sanaa kila mtu ana mipango yake, mimi sikurupuki, nafanya sanaa kwa malengo, hata sasa hivi nipo lokesheni Bagamoyo,” alisema Maya.