Monday, August 18, 2014

NDINGA LA DUDE NGOMA NZITO..INASEMEKANA ILITUMIKA KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI LILILOSABABISHA MAUAJI

Lile ndinga aina ya Toyota Vitz la mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambalo lilidaiwa kutumika kwa ujambazi juzikati, bado lina ugumu wa kuachiwa kutokana na watuhumiwa walioka matwa nalo kuhusishwa na makosa ya mauaji.
Gari ndogo aina ya Toyota Vitz la mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka jeshi la polisi ambacho kiliomba hifadhi ya jina, Dude amekuwa akifuatilia mara kadhaa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama  ‘Mabatini’, Dar, lakini imeshi ndikana kutokana na kosa hilo.
“Hili suala limeshakuwa gumu, si jepesi kama anavyofikiria, hili gari halipati leo wala kesho atasubiri sana maana wale watuhumiwa waliohusika na lile tukio la kutaka kuiba Bajaj ni majambazi sugu, walikuwa wakisakwa kwa kesi ya mauaji,” kilisema chanzo hicho.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ akiwa ngani ya ofisi za Global.
Ndinga hilo lilikamatwa Julai 21, mwaka huu maeneo ya Kijitonyama likiwa na watuhumiwa waliohusika na tukio la wizi wa Bajaj waliojitambulisha kwa majina ya Seif na Longina.