Habari hii ambayo inaonekana kusababisha panic kubwa kwa mashabiki wa muigizaji "Rambo" imepelekea kutumwa kwa salamu za huzuni kutoka kwa mashabiki wake mbalimbali kupitia mtandao wa twitter.
Elinda Hagan @ElindaHaganFollow
I just heard about Sylvester Stallone! Another favorite actor if mine, RIP
Ripoti hizo za kifo cha Rambo zinadai kuwa alipata ajali mbaya ya gari iliyosababishwa na dereva wake aliekuwa amelewa na kutokuona gari kubwa lililokuwa likija mbele yake.
Hii sio maara ya kwanza kwa muigizaji huyo kuuliwa na internet, mwanzoni uvumi mkubwa wa kifo chake ulioripotiwa na Global Associate News zilidai kuwa Rambo alifariki kwa ajali iliyotokana na snowboarding.
Sylvesta Stallon (68) yuko hai na mwenye afya njema. Baada ya "Expendable 3" atakuwa aki-shoot instalment ya 5 ya film yake "Rambo".
Ukiachana na Sylvester Stallon, wengine waliowahi kuzushiwa vifo ni pamoja na Justine Timberlake, Miley Cyrus na Charlie Hunnam