Wednesday, August 27, 2014

UNYAMA...!! KIGOGO ATOROSHA MTOTO, AMLAWITI

INASIKITISHA sana! Wakati watetezi wa haki za binadamu wakizidi kupiga vita matukio ya unyanyasaji wa watoto na wanawake, kigogo mmoja aliyetajwa kwa jina la Moses anadaiwa kumlawiti mtoto, Rose (16) na kumtorosha mwingine aitwaye Diana (12) ambaye ni denti wa darasa la nne.
Mtoto Rose (kushoto) aliyelawitiwa, na mwenzake Diana aliyetoroshwa na kigogo mmoja aliyetajwa kwa jina la Moses.
Kigogo huyo anayesemekana kuwa ni mfanyakazi wa taasisi moja ya serikali iliyopo jijini Dar (jina tunalihifadhi) alidaiwa kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo ndani ya shamba lake.
Tukio hilo lilitokea Agosti 20, mwaka huu maeneo ya Zogowale, Kibaha Pwani ambapo wachunga ng’ombe waliwaona watoto hao wakiwa katika banda peke yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni, walisema walitolewa mkoani Lindi kwa ajili ya kufanya kazi za ndani huku Diana akianika kwamba huyo Moses alimlaghai kuwa angemnunulia nguo jambo ambalo hakulifanya.
Wananchi wakiwasikiliza watoto waliorubuniwa na kigogo Moses.
“Mimi nilichukuliwa mwaka jana na kupelekwa Dar kwa ajili ya kufanya kazi za ndani, baadaye Moses alinitoa na kunihamishia hapa shambani kwake bila kufanya mawasiliano na wazazi wangu kwani sikuwaaga wakati nakuja,” alisema Rose.Akaongeza: “Nilishindwa kuwaambia wazazi wangu kwa sababu alininyang’anya simu halafu akaanza kunilawiti.”
Mjumbe wa  Serikali ya Mtaa wa Jonunga, Mbegu Twaha alisema taarifa za watoto hao alizipokea kutoka kwa wachunga ng’ombe hao hivyo akaamua kwenda kwenye shamba hilo na kuwakuta bandani.
Alisema baada ya kufanya mahojiano na watoto hao alibaini kuwa, Rose alikuwa akilawitiwa na bosi wake, ndipo akaamua kwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Mlandizi kwa ajili ya fomu ya matibabu (PF3) ambayo ilionesha kuwa kweli binti huyo alikuwa akiingiliwa.
kwa ushirikiano na viongozi wengine wa kijiji walifanikisha kuweka mtego  kumnasa mtuhumiwa huyo na kufikishwa polisi ambako alifunguliwa jalada la kesi lenye Kumbukumbu Na. MLA/IR/1066/2014 KULAWITI.