Wednesday, August 27, 2014

BAADA YA KUCHOSHWA NA MAISHA BILA NDOA....MSANII AKOMBA VITU KWA BWANA’KE

MSANII wa filamu Bongo, Fatma Leonard wiki iliyopita alinaswa na paparazi wetu akihamisha vitu vya ndani nyumbani kwa mpenzi wake huko Ubungo Makuburi jijini Dar es Salaam akidai kuchoshwa na maisha bila ndoa. Hata hivyo, gazeti hili lilikuta tayari mzigo wa fenicha umeshaondoka.
Msanii wa filamu Bongo, Fatma Leonard akifungasha virago kuianza safari.
“Nimemvumilia kwa muda mrefu sana, kila siku namkumbusha, sasa inaonekana kama ninalazimisha, nimeamua kuchukua vyangu kwa sababu nimempata mtu mwenye mapenzi ya kweli ambaye yupo tayari kunioa,” alisema Fatma akikataa kulitaja jina la mpenzi wake huyo anayempotezea muda.
Fatma Leonard 'akila kona'.
Msanii Fatma Leonard akiingia kwenye ndinga tayari kwa kusepa.
Baba mwenye nyumba hiyo alimpigia simu mpangaji wake kumfahamisha kuhusu kuondolewa kwa mizigo hiyo, lakini alimtaka amuache achukue anachotaka, kitu kinachoonyesha aliridhia kitendo hicho kilichowavutia majirani wengi waliojazana kushuhudia.