MUIGIZAJI Jacqueline Pentezel maarufu kwa jina la Jack wa Chuz, amefunguka kuwa mume wake, Gadner Dibibi anapenda mwanamke mwenye mwili mkubwa yaani bonge.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, Jack alisema isingekuwa kuilinda ndoa, asingekubali auachie mwili wake aonekane bonge nyanya kiasi hicho alichonacho hivi sasa.
“Napenda sana kumsikiliza mume wangu, chochote anachokihitaji nitakifanya hata kama kipo nje ya uwezo wangu, nitajitahidi tu. Sasa alivyoniambia kuwa anapenda mwili wangu uonekane wenye supu supu na minofu mingi nikakubali ndiyo maana nimejiachia” alisema Jack.